Askari
waliomleta mahakamani mtuhumiwa askari wa FFU mwenye namba G2573
Pasificus Cleophace Simoni (23) wa mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa
habari wa kituo cha Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi,
wamemtibua Hakimu aliyeagiza mtuhumiwa huyo kurudishwa tena kizimbani
hapo kwa kudharau mahakama hiyo.
Tukio hilo lilitokea leo majira ya saa 5.35 lilitokea mara baada ya mahakama hiyo kuombwa kutaja tarehe nyingine ya kutajwa kesi hiyo. Askari watatu, ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja, walimshusha mtuhumiwa kizimbani na kumkimbizia mahabusu kama njia ya kukwepa kupigwa picha na wanahabari waliokuwepo hapo .
Mahakama ikiwa bado inaendelea na shughuli ya keshi hiyo kwa Hakimu Mkazi wilaya ya Iringa, Dyness Lyimo kutaja tarehe ya kesi hiyo, mtuhumiwa alishuka kizimbani huku akivaa kofia yake ya sweta (mzula) na miwani ya giza na kuanza kushuka jukwaani. Hakimu alimtaka mtuhumiwa huyo kutovalia kofia hiyo kizimbani.
Wakati hakimu huyo akijiandaa kusimama ili kuhitimisha shughuli za Kimahakama kwa siku hiyo, ghafla alijikuta anabaki na Mwanasheria waMmahakama, Karani wake, Wanahabari, Askari mmoja na ndugu wawili wa mtuhumiwa, huku askari 3 wenye silaha na mtuhumiwa huyo wakiwa tayari wameondoka ndani ya chumba cha mahakama hiyo.

Mbona hao askari wanamtoa mtuhumiwa bila utaratibu wa mahakama hebu mwanasheria waambie wamrudishe ndani mtuhumiwa ....huu si utaratibu mbona wanafanya fujo mahakamani hao.Pamoja na jitihada za mwanasheria wa serikali Adolf Maganda kuwaita kwa sauti, askari hao kuwataka kumrudisha ndani ya mahakama mtuhumiwa huyo bali walizidi kukimbia na mtuhumiwa kwenda naye mahabusu.
Baada ya dakika kama 5 hivi, ndipo mwanasheria huyo aliporejea na askari hao na mtuhumiwa ambaye hata hivyo hakwenda kusimama kizimbani na badala yake alikwenda upande wa kushoto wa mahakama ambako alikuwa amekaa mwanzoni kabla ya mahakama kuanza na kuketi katika kiti huku akiwa bado amevaa miwani na kofia yake.
Kutokana na tukio hilo, Hakimu huyo alilazimika kuwahoji askari hao watatu kwa vurugu hizo walizozifanya kwa kuwauliza swali moja pekee , ikiwa wanaona walichofanya ni sahihi, ambapo askari hao waliosema, “samahani mheshimiwa”.
Mwendesha mashtaka wa Jamhuri, Adolf Maganda aliiomba mahakama kutaja tarehe nyingine ya kutajwa tena kwa kesi hiyo ambayo awali ilikuwa imetajwa Januari 27, 2013 lakini mtuhumiwa alishindwa kufika Mahakamani kutokana na ugonjwa. Mahakama hiyo imeahirisha kesi hiyo hadi Februari 14 mwaka huu.
Mtuhumiwa huyo anatuhumiwa kumuua kwa makusudi kwa bomu aliyekuwa mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa marehemu Mwangosi septemba 2 Septemba mwaka jana katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa wakati zilipozuka vurugu kati ya Askari Polisi na wafuasi wa CHADEMA.
Habari kwa hisani ya mpekuzi blog
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !