Headlines News :

Powered by Blogger.

Tangaza habari, matangazo na the geeb blog

unasubili nini changamkia offer kwa kutangaza na the geeb blog
Home » , » Inawezekana mwanamke akampelekea mwanamume kuwa muongo katika uhusiano

Inawezekana mwanamke akampelekea mwanamume kuwa muongo katika uhusiano

Written By Gimasa Ruyembe on Saturday, March 2, 2013 | 5:50 PM


Kuna vitu mbalimbali ambavyo wanawake huwa hawapendi kuambiwa ukweli kwa mfano,, unaweza kumkuta mwanamke amevaa nguo vizuri na kujitizama kwenye kioo akaona amependeza lakini atarudi na kumuuliza mpenzi wake mbona hunisifii kama nimependeza?? ikitokea mwanamume akimuambia hajapendeza kwa mtazamo wake basi atanuna kitendo ambacho kitampelekea huyo mwanamume kushindwa kumkosoa wakati mwingine,  atakua anakuambia umependeza wakati haujapendeza ni vizuri kukubali ukweli,, mbali na mavazi kuna mapishi, mwanamume anaweza kukusifia chakula alichopika mwenza wake ni kizuri hata kama ni kibaya alimradi tu amfurahishe mpenzi wake katika hili kuna namna ya kumueleza kwa lugha nzuri ili aweze kujifunza kupika sasa ukimsifia kuwa anajua wakati hajui atajifunza lini.

Ni vyema kwa mwanamke kutambua nini ambacho anakosea ili aweze kutafuta utatuzi na si  kumwambia kuwa yeye ni bora wakati hakuna kitu mfundishe yale anayokosea  na mwanamke inapotokea mpenzi wako anakukosoa basi usilalamike na kuona kuwa hakupendi kaa chini na tafakari ili ujue kipi kilicho sahihi MAPENZI YANAHITAJI USHIRIKIANO PANDE ZOTE MBILI,,Lakini pia kuna ile hali mwanamume ametoka safari au amechelewa kurudi nyumbani unaanza kumuuliza umetoka wapi? akikujibu kuwa ametoka kazini au safari unaanza kulalamika na kusema ni uongo bila kuwa na uhakika na ndiyo maana unakuta wanaume wanasema Baadhi ya wanawake hawapendi kuambiwa ukweli. sijui unalionaje hili mdau ni mtazamo tu.
                                          By the geebtz blogspot.
Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Proudly powered by The Geebtz
Copyright © 2013. the geeb - All Rights Reserved
Original Design by The Geeb