Headlines News :

Powered by Blogger.

Tangaza habari, matangazo na the geeb blog

unasubili nini changamkia offer kwa kutangaza na the geeb blog
Home » » LHRC yalalamikia ukiukwaji haki za binadamu nchini

LHRC yalalamikia ukiukwaji haki za binadamu nchini

Written By Gimasa Ruyembe on Sunday, January 6, 2013 | 3:16 PM



Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk Helen Kijo-Bisimba 
 Kwa ufupi
Hayo yalibainishwa jana jiji Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk Helen Kijo-Bisimba, alipokuwa akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya miaka 64 ya Tamko la Haki za Binadamu Duniani na miaka 10 ya uandishi wa ripoti za haki za binadamu Tanzania.



KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema haki ya kuishi, imekuwa ikikiukwa kwa kiwango kikubwa hapa nchini huku na kwamba ongezeko la vifo vya raia vinavyo sababishwa na vyombo vya usalama, likiwamo Jeshi la Polisi, vimeongezeka kwa kasi hadi kufikia 193 katika kipindi cha kati ya mwaka 2005 na mwaka jana.

Kituo hicho kimesema vyanzo vingine vya raia kukosa haki zao za msingi za kuishi ni pamoja na ajali, adhabu ya kifo, mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, mauaji holela yanayofanywa na vyombo vya usalama.
Hayo yalibainishwa jana jiji Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk Helen Kijo-Bisimba, alipokuwa akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya miaka 64 ya Ttamko la Haki za Binadamu Duniani na miaka 10 ya uandishi wa ripoti za haki za binadamu Tanzania.

Alisema ripoti mbalimbali zilizoandikwa na kituo hicho tangu mwaka 2002, zinaonyesha kuwa mauji ya raia yanayofanywa na vyombo vya usalama, yameongezeka kwa kasi na kufikia vifo 193.

Alisema LHRC wakati inaanza uandishi wa ripoti mbalimbali za haki za binadamu ikiwa pamoja na haki ya kuishi, imebaini kuwapo kwa ongezeko kubwa la mauaji ya raia, jambo ambalo si jema kwani linaondoa misingi ya haki za kuishi kwa binadamu.
“Mwaka 2002 hakukuwa na mauaji yaliyo ripotiwa lakini mwaka 2004 watu nane waliuawa na polisi huko Mbeya, Musoma, Tarime na Dar es Salaam,” alisema Dk Bisimba.

Alisema mauaji hayo yaliendelea na kwamba mwaka 2005 watu 36 waliuawa. Alisema mwaka 2006 watu wengine 37 waliuawa na kufuatiwa na mwaka 2007 ambapo watu 14 waliuawa. Dk Bisimba alisema licha ya mauaji yanayofanywa na polisi, tafiti zinaonyesha kwamba pia kuna mauji yanayofanywa na raia wanaojichukulia sheria mkononi.

“Katika kipindi hiki cha miaka 10, tumebaini sababu mbalimbali lakini kubwa mbili ni wananchi kukosa ulewa wa masuala ya haki za binadamu na sheria, jambo linalosababisha kuamua kujichukulia sheria mkononi,” alisema.

Dk Bisimba alifafanua kwamba miaka inavyo zidi kwenda taarifa mbalimbali zinaonyesha kwamba watu wengi wanaendelea kupoteza maisha kutokana na jambo hilo. 0
                             Habari kwa hisani ya gazeti la Mwananchi
Share


Share this article :

0 comments:

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

 
Proudly powered by The Geebtz
Copyright © 2013. the geeb - All Rights Reserved
Original Design by The Geeb