Habari na mwakilishi wa the geeb kutoka Musoma-mjini-Masau Lucas
Kwa kifupi
Baada ya miezi kadhaa ya hofu,majonzi na mauaji ya kikatili sasa amani imerejeshwa na jeshi la Polisi mkoani Mara;
Wakazi wa mkoa wa Mara sasa wamerejea katika hali yao ya kawaida baada ya miezi kadhaa iliyopita kuwa katika hali ya wasiwasi wakihofia uhai wao baada ya kuzuka kundi ama mtandao uliojulikana kama MAKILIKILI uliokuwa ukichinja watu.. Kundi hili lilichinja watu wa rika zote bila kujali umri, jinsia na hatimae kuchukua baadhi ya viungo vyao. Lakini kwa sasa hali ni shwari kabisa na wakazi wa mkoa wa Mara na vitongoji vyake vyote wanaendelea na shughuli zao za kila siku.
Ni baada tu ya jeshi la Polisi kuwasaka na kuhakikisha mtandao huo uliokuwa unafanya mauaji hayo unakamatwa na wahusika kuchukuliwa hatua kali za kisheria. Wakazi wa mkoa wa Mara wanalishukuru jeshi la Polisi chini ya IGP-MWEMA kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuwasaka na kuwatia mbaroni watuhumiwa wote wa mauaji hayo. Mtandao huo wa mauaji ya kinyama ulikuwa ukiogozwa na diwani wa CCM kata ya Mugango Musoma-vijijini Mheshimiwa Wandwi Kunju Maguru, ambae kwa sasa yuko mikononi mwa Polisi pia amekwisha fikishwa Mahakamani pamoja na mtandao wake na wengine bado uchuguzi unaendelea na wakibainika kuhusika sheria itachukua mkondo wake.
Pamoja na jitihada zote zilizofanyika lakini bado wananchi wa mkoa wa Mara wana wasiwasi ama hawana imani na DC wa Musoma mjini Mheshimiwa Masome ambae alikuwa akipingana na wananchi kwa kusema hakuna mauaji bali ni uvumi tu na atakae bainika akieneza uvumi huo atakamatwa huku wananchi wakiendelea kuuwawa kikatili. kitendo hichokilisababisha wakazi wake kutokua na imani nae pamoja na baadhii ya askari polisi. Aidha wananchi wanaendelea kulalamika kuhusiana na jeshi la Polisi hususani baadhi ya maaskari wa Musoma mjini kuwa si waadilifu, kwani wengi wao wanamiliki mali nyingi kupita kipato chao hii inawapa hofu wakazi wa mkoa wa Mara wakiamini huenda wanajihusisha na vitendo vya uhalifu.
Wananchi wanaiomba serikali kuwachunguza askari wote wa Musoma mjini na iwapo watabaini kuwapo maaskari wasio waadilifu basi wachukuliwe hatua za kisheria ili kurejesha imani ya jeshi la Polisi kwa wananchi.
Mwisho kabisa the geeb blog inawapa pongezi wale wote kwa namna moja au nyingine wameshiliki kikamilfu kuhakikisha mtandao wa MAKILIKILI unateketezwa.
Tutaendelea kuwaletea habari zaidi kuhusiana na kesi ya mtandao wa MAKILIKILI.
Home »
Baada ya miezi ya mauaji MUSOMA amani yarejea.
» Baada ya miezi ya mauaji MUSOMA amani yarejea.
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !