Kwanza niwape pole sana watanzania wezangu wapenzi wa tasnia ya filamu nchini kumpoteza msanii wa nguli wa filamu Juma Kilowoko almaarufu kama SAJUKI!japokuwa kifo ni kazi ya mungu lakini hata binadamu wanaweza kusababisha kwa namna moja au nyingine kwa mfano kwa kumpa sumu,kumpiga kumgonga na gari nk.Na pia si utamaduni mzuri kutupiana lawama baada ya kutokea kifo cha mpendwa au wapendwa wetu!Kuna habari zisizo rasmi zinazosema bongo movies waliharibu tamasha la marehemu aliloandaa huko Arusha kwa ajili ya kukusanya fedha za matibabu yake nchini India!naasikia baada ya kupata taarifa hizo ndipo alipopata mshituko na kuanguka chini na kuzidiwa mpaka kupelekwa Dsm!Lakini pia bongo movies haohao walishindwa kushughulikia kwa haraka kupeleka barua ikulu ili wapatiwe msaada wa kumpeleka sajuki nchini India!kwa kuwa Jk alishakubali kugharamia
matibabu ya sajuki ila ilihitajika tu barua kwenda ikulu. swali la kujiuliza hapa kwa nini Ikulu walihitaji barua wakati hali ya mgonjwa ishaanza kuwa mbaya au ndo itifaki lazima izingatiwe?Pengine Sajuki angewahishwa kupelekwa India labda kifo chake kisingeweza kutokea. Najua tutayasikia mengi sana baada ya kifo cha msanii huyu lakini yote kwa yote ni kwamba Sajuki ametutangulia mbele za haki ila kifo chake kiwe ni funzo kubwa kwa wasanii wa Tanzania, najua sasa hivi watakuwa bize madukani kutafuta suti, miwani nyeusi,madira ya gharama kubwa kwa ajili ya kwenda kuuzia sura kwenye msiba na wengine watakuwa wapo salon wakifanya scrabing na make up ili watokelezee kwenye ma-TV!MWISHO NITOE POLE ZA DHATI KABISA KWA MKE WA MAREHEMU SAJUKI WASTARA KWA KUPIGANIA MAISHA YA MUMEWE MPK DAKIKA YA MWISHO BILA KUCHOKA TENA KWA UJASIRI MKUBWA! MWENYEZI MUNGU AMJALIE MOYO WA SUBIRA NA AMPE NGUVU KTK KIPINDI HIKI KIGUMU ANACHOPITIA KTK MAISHA YAKE!Mwenyezimungu ailaze roho ya marehemu SAJUKI mahali pema peponi AMEN.