0
inShareHALI ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya
Jinai wa Jeshi la Polisi (DCI), Kamishna Robert Manumba ni mbaya na
amelazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU), Hospitali ya Aga
Khan, Dar es Salaam.Habari zilizopatikana jana zilieleza kuwa
Manumba amelazwa hospitalini hapo baada ya kusumbuliwa na maradhi
kadhaa, ikiwamo figo.Taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi
zilisema jana kuwa tangu juzi, Manumba alikuwa hajitambui baada ya
kuugua malaria ghafla na hali hiyo ilisababisha pia figo zake zote mbili
kushindwa kufanya kazi.“Alitakiwa kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu,
lakini ilishindikana kwa sababu hajitambui, wakajaribu kumzindua,
ikashindikana,” kilieleza chanzo hicho cha habari ndani ya jeshi hilo.Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso,
alithibitisha kamishna huyo kulazwa ICU Aga Khan lakini akasema kuwa
hadi jana jioni, hali yake ilikuwa ikiendelea vizuri.“Ni kweli amelazwa katika hospitali ya Aga Khan, lakini hali yake inaendelea vizuri,” alisema Senso.
Mtu
wa karibu na Manumba, alisema, Manumba alikutwa na vijidudu 500 vya
malaria, tatizo ambalo lilisababisha pia viungo vyake vingi, ikiwamo
figo kushindwa kufanya kazi“Kutokana na hali aliyonayo tumeshindwa
kumsafirisha kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu zaidi kwa sababu
baadhi ya viungo havifanyi kazi,” alisema mtu huyo.
Hata hivyo, alisema hali ya Manumba inaendelea vyema baada ya kuanza kupata matibabu.
JK amjulia hali
Viongozi
mbalimbali wa Serikali, akiwamo Rais Jakaya Kikwete jana walifika
hospitalini hapo kumjulia hali kamishna huyo wa polisi.
Habari
zilizopatikana zilieleza kuwa Rais Kikwete alifika hospitalini hapo jana
mchana baada ya kumsindikiza mgeni wake, Rais wa Benin ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Boni Yayi.
Daktari Mganga
Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan, Dk Jaffer Dharsee alisema jana kwamba
Manumba alifikishwa katika hospitali hiyo tangu juzi akisumbuliwa na
malaria na alikuwa hajitambui.Dk Dharsee alisema kuwa uchunguzi wa awali
ulionyesha kwamba alikuwa na malaria kali iliyosababisha alazwe ICU.
Hata hivyo, alisema baada ya matibabu, hali yake ilianza kubadilika na
kuleta matumaini.
“Nimepigiwa simu nyingi leo (jana), nikiulizwa
na watu mbalimbali wakitaka kufahamu kama Manumba amefariki dunia,
ninachotaka kuwaambia ni kwamba ni mzima lakini yuko ICU,” alisema.
Habari kwa hisani ya gazeti la Mwananchi
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !