Mkuu wa
Wilaya ya Kilindi, Suleiman Liwowa, ameanza kuwachukulia hatua baadhi ya
viongozi wanaotuhumiwa kuhusika na uvunjaji wa amri halali ya Mkuu wa
Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa, ya kuzuia ukataji miti na ugawaji ardhi
kwa kumtia mbaroni Diwani wa Kata ya Pagwi (CCM). “Tumeanza
kuwashughulikia, juzi nilimuweka ndani Diwani wa Kata ya Pagwi kwa
sababu anafahamu kwamba serikali imepiga marufuku ugawaji wa ardhi.
Lakini tumekuta eneo ambalo miti imeteketezwa na tumeelezwa hilo shamba
ni lake. Pia hata majirani zake nao ni wageni wamepewa ardhi hivi
karibuni,” alisema Liwowa na kuongeza: “Sasa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya tumekaa na tukapata uamuzi wa kumshitaki.
Habari kwa hisani ya Chingaone blog
0 comments:
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !